Historia inajionesha ya kwamba kiasi cha miaka 20,000 kumekuwepo
makazi ya bidadamu katika visiwa vya Zanzibar. Visiwa hivi ni sehemu ya
kumbukumbu ya kihistoria ya ulimwengu wakati waajemi wafanyabiashara
waliigundua na kufanya ndio makao makuu kwa safari kati ya Mashariki ya
Kati, India, Na Afrika.
Katika karne ya mwanzo AD Zanzibar pamoja na mwambao wa Afrika ya
Mashariki ulikua katika ufalme wa Saba,Katika kipindi cha karne ya 3 na
4AD,Wabantu walianza biashara na Waarabu waliokuja Afrika ya Mashariki.
Katika karne ya 7 AD,waarabu walikuja Zanzibar kibiashara pia kusambaza
Dini ya Kiislam,Waarabu ndio waliyoipa jina ZANZIBAR kutokana na neno la
Kiarabu ZINJI BAR yaani sehemu ya watu weusi.
Lugha ya kiswahili imeanza kutumika kiasi cha karne ya 13 AD,Lugha ya
kiswahili ilitokana na kuchanganyika lugha ya kiarabu na lugha za
kiafrika.
Karne ya 16 AD wareno walikuja Zanzibar lakini utawala wao ulifuatiwa
na kutokuwepo utulivu,lakini biashara ya Utumwa iliwaweka watu pamoja.
Waarabu kutoka Oman walichukua utawala Zanzibar katika karne ya 17 AD,Na
Zanzibar ilikua ni makao makuu ya utawala wa Waomani.
1820-1870 Zanzibar ilifaidi matunda mazuri ya kiuchumi na maendeleo
yaliyosababishwa na utawala wa kisultani na hivyo kupelekea Zanzibar
kuwa na mwakilishi nchini marekani na kupelekea kuenea kwa Dini ya wa
kiislam. Katika karne ya 19 AD Zanzibar ilikua chini ya utawala wa
Oman,mwaka 1830 Zanzibar ilikua inaongoza kwa kilimo cha karafuu ,na
hiyo kupelekea mahitaji ya watumwa kuongezeka kutumika katika kilimo.
1885 kamisheni kutoka Uengereza na Ujerumani iliamua kuigawa Zanzibar
kutoka katika utawala wa Kisultani na ndio ulikua mwisho wa utawala wa
kujitegemea kwa Zanzibar na mnamo mwaka 1886 sultani alikubali
maridhiano hayo.
1890 Zanzibar ilikua chini ya uangalizi wa waingereza rasmi lakini
uchaguzi wa mwanzo ulifanyika mwaka 1957,na miaka iliyofuata kukakuwepo
fujo na machafuko kutoka kwa waafrika wanaodai uhuru dhidi ya utawala wa
kiarabu. Mwezi wa 12 mwaka 1963 Waingereza waliipa uhuru Zanzibar chini
ya jumuiya ya madola,na mwezi wa mwaka 1964 Zanzibar ilifanya mapinduzi
kujikomboa kutoka katika utawala wa kisultani,muda mchache baadae
iliungana na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA.
No comments:
Post a Comment